MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Ureno na klabu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo sio pekee katika familia yao anayeweza kusaini mkataba wa kuvunja rekodi jijini Madrid katika kipindi hiki cha majira ya kiangazi. Kwani dada yake aitwaye Katia Aveiro naye amepata mkataba mnono na kampuni iliyowatoa kimuziki nyota wengine kama Lady Gaga na Jennifer Lopez ili kusimamia albamu yake ya kwanza. Mwanamuziki huyo ambaye singo yake iitwayo “Boom sem parar” imevuta hisia za mashabiki wengi katika mtandao wa youtube kwasasa atakuwa akifanya kazi chini ya watengenezaji wa kampuni ya RedOne iliyopo jijini Madrid mahali ambako anaishi mwanadada huyo. Kwa upande mwingine mawakala wa kaka yake wanakaribia kufikia makubaliano ya mkataba mpya wa miaka mitano na Real Madrid ambao utamuwezesha kulipwa kiasi cha euro milioni 17 baada ya kukatwa kodi. Kama mkataba huo ukisainiwa Ronaldo atakuwa amevunja rekodi na kuwa mchezaji soka anayelipwa zaidi na kumpita Lionel Messi wa Barcelona ambaye ndio anashikilia rekodi hiyo kwasasa baada ya kusaini mkataba mpya wa miaka mitano. Akizungumzia kuhusu mafanikio ya dada yake katika muziki katika kipindi hiki cha majira ya kiangazi Ronaldo amesema ana furaha sana kwa hatua ya mafanikio aliyopata ndugu yake huyo na kumtakia heri katika safari yake.
Aveiro anategemewa kuimba katika tamasha kubwa jijini Madrid Septemba mwaka huu huku albamu yake ikitarajiwa kuingia sokoni Novemba.
Aveiro anategemewa kuimba katika tamasha kubwa jijini Madrid Septemba mwaka huu huku albamu yake ikitarajiwa kuingia sokoni Novemba.

No comments:
Post a Comment