Tuesday, August 6, 2013

BARCELONA WASAHAU KUHUSU LUIZ - MOURINHO.

MENEJA wa klabu ya Chelsea, Jose Mourinho amewapasha Barcelona ambao walitaka kumsajili beki wake David Luis katika kipindi hiki cha usajili wa majira kiangazi kuwa mchezaji huyo yuko katika mipango yae ya msimu ujao hivyo hawezi kuondoka. Kulikuwa na tetesi zimezagaa mwezi uliopita kuwa Barcelona walikuwa wakimfukuzia beki huyo wa kimataifa wa Brazil na tayari walikuwa wamemtengea kitita cha euri milioni 29. Lakini Mourinho alimaliza uvumi huo kwa kudai kuwa Luis mwenye umri wa miaka 26 yuko katika mipango yake pamoja na kutomtumia katika mechi ya kirafiki dhidi ya AC Milan ambapo waliibuka na ushindi wa mabao 2-0. Mourinho amesema beki huyo yuko katika kiwango kizuri ambacho kitakuwa mchango mkubwa katika kikosi chake hivyo hana sababu ya kumuuza kwasababu atamtumia msimu ujao kuimarisha safu yake ya ulinzi.

No comments:

Post a Comment