KOCHA wa timu ya taifa ya Brazil, Luis Felipe Scolari ametoa wito kwa beki wa zamani wa klabu ya Bayern Munich Breno kuachiwa kutoka gerezani. Breno mwenye umri wa miaka 23 alihukumiwa miaka mitatu na miezi tisa jela JUlai mwaka jana baada ya kukutwa na hatia ya kusababisha moto, lakini Scolari ameziomba mamlaka zinazohusika nchini Ujerumani kumruhusu kurejea nyumbani ili kujaribu kupanga upya maisha yake. Scolari amesema kila binadamu anafanya makosa na katika kipindi ambacho amekaa lupango atakuwa amejifunza hivyo mamlaka zinazohusika nchini zinapaswa kuangalia uwezekano kwa kumpa nafasi nyingine. Beki huyo wa kimataifa wa Brazil ambaye alicheza mechi 21 akiwa na Bayern baada ya kutoka Sao Paulo mwaka 2008 alihikumiwa mwaka jana baada ya tukio la kuchoma nyumba yake aliyopanga jijini Munich Septemba mwaka 2011.

No comments:
Post a Comment