Tuesday, August 6, 2013

MASHABIKI WA SOKA ZAIDI 130 WAHUKUMIWA MOROCCO KWA VURUGU.

VYOMBO vya habari nchini Morocco vimeripoti kuwa watu zaidi 130 wanaotuhumiwa kufanya vurugu mitaani kabla ya mechi ya soka jijini Casablanca, wamehumiwa miaka mitatu jela. Ni watu watatu pekee kati ya 134 ndio walioachiwa huru na mahakama ya rufani ya Casablanca wakati 17 walihukumiwa kutumikia vifungo vya kati ya miezi sita mpaka miaka mitatu. Katika taarifa hiyo imedai kuwa watu hao walihikumiwa kwa kuhatarisha hali ya usalama na kuaribu miondombinu ya jumuiya na binafsi baada ya vurugu hizo zilizotokea kabla ya mchezo kati ya timu ya Raja Casablanca na FAR Rabat April 11 mwaka huu. Hii ni mara ya kwanza kwa mashabiki kusimamishwa mahakamani kutokana na vurugu za soka lakini matukio ya vurugu yanayosababishwa na mashabiki wa soka nchini Morocco imekuwa ni vitu vya kawaida hususani wakati wa mechi za mahasimu kati ya Wydad Casablanca na Raja ambazo zote zinatoka katika mji mkuu wan chi hiyo. Bunge la Morocco limedai kuwa litafanya marekebisho ya adhabu kwa vurugu zinazotokea viwanjani ambapo hukumu yake itapandishwa mpaka kufikia miaka mitano gerezani.

No comments:

Post a Comment