KIUNGO mahiri wa klabu ya Liverpool, Steven Gerrard amemtaka Luis Suarez kubakia klabuni hapo ikiwa ni mwaka mmoja umepita toka Gerrard mwenyewe kukataa kuondoka kwenda kwenye timu inayoshiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Akiongea kabla ya mchezo dhidi ya Olimpiacos katika Uwanja wa Anfield, Gerrard alibainisha kuwa alikuwa na nafasi ya kujiunga na klabu inayoshiriki michuano ya Ulaya msimu uliopita na kumsisitizia Suarez hatakiwi kufanya maamuzi ya haraka kuondoka Liverpool. Gerrard amesema mshambulijai huyo nyota wa Uruguay mwenye umri wa miaka 26 hatakiwi kuwa na haraka kwani ofa kubwa zaidi zitamiminika kwa ajili yake kama akiendelea kubakia Liverpool kwa msimu mwingine mmoja. Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 33 aliendelea kudai kuwa Suarez anastahili kucheza katika moja vilabu vikubwa kabisa kama Real Madrid au Barcelona hivyo akisubiri hakuna shaka kwamba watamuita katika kipindi kifupi kijacho.
No comments:
Post a Comment