Saturday, August 3, 2013

MSIMU MPYA WA SOKA UJERUMANI WAANZA.

MSIMU mpya wa soka bara la Ulaya unakaribia kuanza kuanza rasmi tena huku tayari nchi kama Ujerumani mechi za duru ya kwanza ya Kombe la Shirikisho zimeanza. Michuano hiyo inazishirikisha timu kutoka Ligi Kuu maarufu kama Bundesliga hadi timu za daraja ya sita na mara nyingi mechi hizo hazikosi kuacha mshangao. Mwishoni mwa iki hii kutakuwa na mechi 32 zitakazochezwa ambapo mwaka jana Bundesliga ziliangushwa na timu za daraja za chini katika duru ya kwanza. Mashabiki katika mechi hizo watapata fursa ya kuona wachezaji wapya waliosajiliwa katika timu zao huku timu vigogo kama Bayern Munich, Borussia Dortmund na Bayern Liverkusen zikitegemewa kufanya vyema na kusonga mbele katika michuano hiyo. Fainali ya michuano hiyo kama kawaida huwa inaandaliwa katika uwanja wa Olimpiki mjini Berlin na itachezwa Mei mwakani.

No comments:

Post a Comment