Tuesday, August 6, 2013

HAKUNA MCHEZAJI MPYA ANAYEWANIWA NA BAYERN - RUMMENIGGE.

MWENYEKITI wa klabu ya Bayern Munich, Karl Heinz Rummenigge ameweka wazi kuwa klabu hiyo haina mpango wa kusajili mchezaji mwingine katika kipindi hiki cha usajili wa majira ya kiangazi. Mabingwa wa Ligi ya Mabingwa barani Ulaya, tayari wameshawasajili Jan Kirchhoff, Mario Gotze na Thiago Alcantara kwa ajili ya kampeni yao ya msimu wa 2013-2014 huku kukiwa na tetesi kuwa wanamhitaji pia beki wa Chelsea, David Luis. Hatahivyo Rummenigge kama ilivyokuwa kwa Guardiola alivyosema wiki iliyopita, yeye pia athibitisha kuwa hakuna ukweli wowote kuhusu suala la Luiz na hawataongeza mchezaji yoyote tena katika kikosi chao. Bayern ilifanikiwa kusonga mbele kwa urahisi katika michuano ya DFB-Pokal baada ya kuigaragaza timu ya daraja la pili ya Schwarz-Weiss kwa mabao 5-0 huku kiungo wake nyota Thomas Muller akifunga mabao matatu peke yake.

No comments:

Post a Comment