Wednesday, August 7, 2013

SUAREZ AWAPASHA LIVERPOOL.

HATIMAYE mshambuliaji nyota wa klabu ya Liverpool, Luis Suarez amefunguka na kutaka kuruhusiwa kuondoka Liverpool huku akiwatuhumu waajiri wake kutoheshimu ahadi waliyowekeana. Baada ya vuta nikuvute ya kipindi kirefu kuhusu muskabali wake, nyota huyo wa iimataifa wa Uruguay ameweka bayani nia yake kwa kuipasha Liverpool kuwa nataka kuhamia timu inayoshiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa kama Arsenal ambayo ndio timu pekee mpaka sasa iliyotoa ofa ya kumsajili. Suarez anajiandaa kuwasilisha barua ya kuomba kuondoka mwishoni mwa wiki hii ili kutimiza malengo yake huku akidai kuwa anaungwa mkono na PFA huku pia akijiandaa kufungua mashitaka kwenye bodi ya Ligi Kuu ili imruhusu kuondoka. Nyota huyo mwenye miaka 26 ilibaki kidogo ajiunge na Juventus msimu uliopita lakini amesema alibaki kwa heshima ya Liverpool na kukubaliana kama timu itashindwa kufuzu michuano hiyo angeruhusiwa kuondoka.

No comments:

Post a Comment