Friday, August 9, 2013

I AM NOT A "SUPER TRAINER" - GUARDIOLA.

MENEJA mpya wa klabu ya Bayern Munich, Pep Guardiola amejaribu kupunguza matarajio ya wengi kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa Ligi Kuu nchini Ujerumani kwa kusisitiza kuwa yeye sio mkufunzi aliyebobea. Msimu uliopita Bayern ilifanikiwa kushinda taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya, Bungesliga na DFB-Pokal na kupoteza michezo mitatu pekee katika kampeni yao wakiwa chini ya kocha Jupp Heynckes. Guardiola mwenyewe alipata mafanikio makubwa katika kipindi cha miaka minne ambayo amekuwa akiinoa klabu ya Barcelona lakini wakati akianza kazi yake mpya Allianz Arena amesisitiza kuwa asichuliwe kama mkufunzi aliyebobea kupita wote. Guardiola amesisitiza kuwa kushinda kila mechi sio kazi rahisi na watu wanaamini kuwa watakuwa wakishinda mabao 6-0 au 7-0 lakini kitu hicho hakitawezekana. Kocha amedai kuwa anajua kwamba mashabiki wanataka ushindi zaidi na zaidi lakini amekuwa amekuwa na kikosi hicho katika kipindi cha wiki sita au saba hivyo anahitaji muda zaidi kwasababu yeye ni mwalimu wa kawaida kama ilivyo kwa wengine.

No comments:

Post a Comment