Tuesday, August 20, 2013

KLOSE APANGA KUTUNDIKA DALUGA MWAKANI.

MSHAMBULIAJI nyota wa klabu ya Lazio, Miroslav Klose amebainisha kuwa ana mpango wa kustaafu soka la kimataifa baada ya michuano ya Kombe la Dunia 2014. Nyota huyo mkongwe ambao yuko nyuma kwa bao moja kufikia rekodi ya Gerd Muller ya mabao 68 katika timu ya taifa ya Ujerumani aliondoka Ujerumani mwaka 2011 kuelekea Lazio ambako ameendelea kung’aa katika ushambuliaji pamoja na umri wake kuwa miaka 35. Klose amekiri kufikiria suala la kutundika daluga baada ya michuano hiyo itakayofanyika Brazil na kusisitiza kuwa kombe hilo ni muhimu kushinda kwa Ujerumani kuliko kufikiria rekodi binafsi. Mshambuliaji huyo wa zamani wa Bayern Munich amedai kuwa kwasasa hana mipango yoyote lakini amebainisha kuwa ana nia ya kurejea Bundesliga kutoka Serie A hapo baadae.

No comments:

Post a Comment