RUFANI ya klabu ya Fenerbahce kupinga adhabu ya kufungiwa miezi miwili kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa tuhuma za kupanga matokeo inatarajiwa kuanza kusikilizwa saa chache kabla ya kuanza kwa mchezo wao wa mkondo wa kwanza kufuzu michuano hiyo dhidi ya Arsenal. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Michezo-CAS imedai kuwa wataanza kuanza kusikiliza rufani hiyo kupinga adhabu iliyotolewa na Shirikisho la Soka barani Ulaya-UEFA, Jumatano na Alhamisi ya wiki hii. Mbali na kusikiliza rufani ya Fenerbahce, CAS pia watasikiliza rufani ya klabu ya Besiktas ambayo nayo inakabiliwa na tuhuma kama hizo za kupanga matokeo katika mechi zao za Ligi Kuu nchini Uturuki. CAS inatarajiwa kutoa uamuzi wake baada ya kusikiliza rufani hizo Agosti 28 kwa Fenerbahce na Agosti 30 kwa Besiktas.
No comments:
Post a Comment