Tuesday, August 20, 2013

MAJERUHI WAIANDAMA SAFU YA ULINZI YA PELLEGRINI.

MENEJA wa klabu ya Manchester City Manuel Pellegrini anakabiliwa na matatizo makubwa katika safu ya ulinzi wa kikosi chake baada ya Micah Richards kupatwa na majeraha ya msuli katika mazoezi ya timu hiyo Jumatatu. Richards mwenye umri wa miaka 25 anatarajiwa kufanyiwa uchunguzi zaidi kutokana na tatizo alilopata huku akitarajiwa kukaa nje ya uwanja kwa kipindi cha wiki tatu au zaidi. Beki huyo anaungana na Vincent Kompany katika orodha ya majeruhi baada ya nahodha huyo wa City naye kuumia katika mchezo dhidi Newcastle ambao walishinda ka mabao 4-0. Pellegrin alikuwa akilijua kwamba wanaweza kupungukiwa na mabeki mapema katika kipindi hiki cha usajili wa majira ya kiangazi lakini walishindwa kumsajili beki wa Real Madrid, Pepe ili aweze kuimarisha safu yake hiyo.

No comments:

Post a Comment