TIKETI kwa ajili ya kushuhudia michuano ya Kombe la Dunia 2014 nchini Brazil zimeingia sokoni rasmi jana huku mashabiki wa soka wakiwa na uwezo wa kuweka oda zao kupitia mtandao wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA. FIFA inategemea mahitaji sawa kama ilivyokuwa katika michuano hiyo nchini Ujerumani mwaka 2006 ambayo kulikuwa na watu saba waliohitaji katika kila tiketi za mechi 64 za michuano hiyo. Zaidi ya tiketi milioni 3.3 zinatarajiwa kuwepo kwa ajili ya michuano hiyo ambayo huchezwa mara moja katika kila miaka minne. Gharama za tiketi zinakadiriwa kuwa dola 90 kwa mechi za mzunguko wa kwanza na kufikia dola 990 kwa mechi ya fainali itakayofanyika katika Uwanja wa Maricana uliopo jijini Rio de Janeiro. Raia wa Brazil wenye umri unaozidi miaka 60, wanafunzi na baadhi ya wafanyakazi wa mashirika ya kijamii wanaweza kununua tiketi hizo kwa dola 15.
No comments:
Post a Comment