Thursday, August 22, 2013

SHARAPOVA AJITOA US OPEN.

MWANADADA nyota katika tenisi, Maria Sharapova wa Urusi amejitoa katika michuano ya wazi ya Marekani inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi wiki ijayo kutokana na kupata majeraha ya bega. Sharapova ambaye ni bingwa wa michuano hiyo mwaka 2006 aliumia bega lake la kulia wakati wa mazoezi. Mwanadada huyo mwenye umri wa miaka 26 aliandika kuthibitisha taarifa katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa facebook na kudai amejitahidi ili aweze kupona haraka lakini imeshindakana ndio maana ameamua kujitoa. Sharapova amesema amefanya vipimo kadhaa na kupata ushauri kutoka kwa watu mbalimbali na ameona atoe muda zaidi ili bega yake liweze kupona kabisa.

No comments:

Post a Comment