Thursday, August 22, 2013

KUUMIA KWA MESSI PIGO BARCELONA.

KLABU ya Barcelona imethibitisha kuwa mshambuliaji wao nyota Lionel Messi alipata majeraha katika mguu wake wa kushoto katika mchezo wa Super Cup dhidi ya Atletico Madrid ambao uliisha kwa sare ya bao 1-1. Messi alitolewa na nafasi yake kuchukuliwa na Cesc Fabregas katika kipindi cha mapumziko kwenye mchezo huo wa mkondo wa kwanza uliofanyika katika Uwanja wa Vicente Calderon. Katika taarifa iliyotumwa katika mtandao wa klabu hiyo imedai kuwa Messi alitolewa kwa ajili ya tahadhari kutokana na maumivu aliyopata yaliyotakana na kugongana. Nyota huyo wa kimataifa wa Argentina amekuwa akisumbuliwa na misuli ya mguu wake wa kushoto wiki iliyopita lakini aliruhusiwa kucheza katika mchezo wa ufunguzi wa La Liga ambao Barcelona ilishinda kwa mabao 7-0 dhidi ya Levante.

No comments:

Post a Comment