Thursday, August 1, 2013

MCHEZAJI WA TAHITI ASHINDWA VIPIMO VYA DAWA ZZILIZOPIGWA MARUFUKU.

SHIRIKISHO la Soka Duniani-FIFA limemsimamisha mchezaji wa timu ya taifa ya Tahiti kwa siku 30 baada ya kushindwa vipimo vya madawa ya kuongeza nguvu katika michuano ya Kombe la Shirikisho. Katika taarifa yake FIFA haikumtaja mchezaji huyo wala kuelezea kwa undani suala hilo lakini ilidai kuwa mchezaji huyo alichukuliwa vipimo baada ya Tahiti kufungw ana Uruguay mabao 8-0 jijini Racife Juni 23. FIFA imeeleza kuwa itafungua kesi ya kinidhamu na kumuoita mchezaji huyo kujibu tuhuma hizo zinazomkabili. Hilo ni tukio la tatu kwa wachezaji kushindwa vipimo hivyo katika mechi za FIFA huku tayari shirikisho hilo machi mwaka huu likiwa limeshamfungia miaka miwili kiungo wa kimataifa wa Peru Joel Sanchez kwa kukutwa ametumia dawa hizo kwenye mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Bolivia Octoba mwaka jana. Wiki iliyopita Shirikisho la Soka la Jamaica lilidai kuwa mchezaji wake mmoja alishindwa vipimo vya dawa za kuongeza nguvu baada ya mechi dhidi ya Honduras iliyochezwa Juni mwaka huu.

No comments:

Post a Comment