Thursday, August 1, 2013

HATUNA MPANGO WA KUMUUZA MODRIC - ANCELOTTI.

MENEJA wa klabu ya Real Madrid, Carlo Ancelotti amesisitiza kuwa hana mpango wa kumuuza kiungo wake mahiri Luka Modric katika kipindi hiki cha usajili wa majira ya kiangazi. Kiungo huyo wa kimataifa wa Croatia ni mmoja wa viungo David Moyes anaowahitaji kama Manchester United ikishindwa kumsajili Cesc Fabregas wa Barcelona katika kipindi hiki cha kiangazi. Modric ambaye alijiunga na Madrid akitokea Tottenham Agosti mwaka jana amecheza mechi 33 za La Liga msimu uliopita chini ya Jose Mourinho na Ancelotti amesema kiungo huyo mwenye miaka 27 yuko katika mipango yake kwa ajili ya msimu mpya. Ancelotti amesema wachezaji wote wanafuraha kuwepo hapo na kufanya kazi pamoja naye na kudai kuwa hawajazungumza na mchezaji yoyote kuhusu kuondoka hivyo Modric hawezi kwenda popote.

No comments:

Post a Comment