Thursday, August 1, 2013

HATIMAYE TOTTENHAM WALEGEA NA KUMUACHIA BALE.

KLABU ya Real Madrid ya Hispania wanaamini kuwa hatimaye wameweza kuishawishi klabu ya Tottenham Hotspurs kumuuza mshambuliaji wake Gareth Bale kwa ada ya paundi milioni 87 ambayo itavunja rekodi ya dunia. Baada ya kupita wiki kadhaa wakisisistiza kuwa Bale hauzwi, Spurs wameonekana kulegea na kukubali kumuachia nyota huyo wa kimataifa kutoka Wales. Kuna tetesi kuwa Spurs wamekubali kumuachia nyota huyo kwa masharti kwamba mpaka watakapomaliza kuwasajili wachezaji wanaowahitaji ndio habari hizo zitangazwe hadharani. Spurs kwasasa inategemea kukamilisha usajili wa Roberto Soldado uliowagharimu paundi milioni 26 kutoka Valencia na meneja wa klabu hiyo Andre Villas-Boas pia anamnyatia kinda lenye miaka 20 Alvaro Morata kutoka Madrid.

No comments:

Post a Comment