Monday, August 19, 2013

PISTORIUS KUFIKISHWA MAHAKAMANI.

MWANARIADHA nyota mlemavu Oscar Pistorius wa Afrika Kusini anatarajiwa kuonekana mahakamani tena jijini Pretoria kwa ajili ya kesi ya kumuua mpenzi wake reeva Steenkamp inayomkabili. Upande wa mashitaka unatarajiwa kuwasilisha mashitaka ya mauaji ya rafiki wa kike wa mwanariadha huyo huku tarehe ya kesi nayo ikitarajiwa kupangwa. Pistorius mwenye umri wa miaka 26 alikana tuhuma hizo za kumuua kwa makusudi Reeva Steenkamp akidai kuwa alimpiga risasi kwa bahati mbaya akidhani alikuwa jambazi aliyevamia kwake. Tukio la kukamatwa kwa Pistorius liliwashtusha wananchi wengi wa Afrika Kusini ambao walikuwa wakimchukulia mwanariadha huyo kama shujaa baada ya kupambana kwa kipindi kirefu na kufanikiwa kushiriki michuano ya olimpiki akiwa mlemavu.

No comments:

Post a Comment