HUKU kukiwa na sintofahamu juu ya mstakabali wa Wayne Rooney, meneja wa klabu ya Manchester United David Moyes amedai kuwa hana mpango wa kumpigia magoti mshambuliaji huyo ili abakie Old Traford. Akiulizwa jinsi gani Rooney alivyochukulia suala la United kukataa ofa ya paundi milioni 30 kutoka kwa Chelsea, Moyes alijibu kwa kifupi hafamu na wala hajamuuliza kuhusiana na hilo. Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya mchezo wa kirafiki ambao United ilitoa sare ya kufungana na bao 1-1 na AIK jijini Stockholm, Sweden, Moyes amesema kuwa hana haja ya kumshawishi mchezaji yoyote kuichezea timu yake. Kauli hiyo kutoka kwa Moyes inaweza kuongeza moto zaidi kwa Rooney ambaye ameshaomba mara mbili kuondoka kuona kama hahitajiki klabuni hapo.

No comments:
Post a Comment