KIUNGO mahiri wa kimataifa wa Ivory Coast Yaya Toure ametajwa kuwa mchezaji bora wa mwaka wa nchi hiyo katika msimu wa 2012-2013 baada ya kupata asilimia 32 ya kura zilizopigwa na waandishi wa habari za michezo na watumiaji wa mtandao. Toure mwenye umri wa miaka 30 anayecheza katika klabu ya Manchester City anafuatia na mshambuliaji nyota wan chi hiyo Didier Drogba aliyepata asilimia 24 wakati nafasi ya tatu inashikiliwa na Bony Wilfried aliyepata asilimia 17. Wengine ni Aroune Kone ambaye amejiunga na timu ya Everton akitokea Wigan mwezi uliopita pamoja na Gervino aliyejiunga na AS Roma akitokea Arsenal ambao wote kwa pamoja wamepata asilimia 15 ya kura zilizopigwa. Hiyo inakuwa mara ya tatu Toure kushinda tuzo hiyo mara nyingine ikiwa mwaka 2008 na 2009.
No comments:
Post a Comment