KLABU ya Anzhi Makhachka ya Urusi imewaweka wachezaji wake wote nyota katika orodha ya uhamisho akiwemo nahodha wake Samuel Eto’o. Miezi miwili iliyopita Eto’o aliambiwa na uongozi wa klabu hiyo kuwa mshahara wake wa paundi 350,000 kwa wiki utakatwa mara tatu kama akiamua kubakia klabuni hapo. Mbali na Eto’o mwenye umri wa miaka 32, wachezaji wengine wanaolipwa zaidi kama Willian wa Brazil na Lassana Diarra wote wameingizwa sokoni baada ya rais wa klabu hiyo Suleiman Kerimov kutangaza kupunguza gharama za uendeshaji kwa asilimia 60. Dhumuni la kupunguza wachezaji wenye majina makubwa ni kuruhusu klabu hiyo kujijenga kupitia shule yao ya michezo baada ya kushindwa kupata mafanikio waliyoyataka toka mwaka 2011.
No comments:
Post a Comment