WAKALA wa beki wa klabu ya Liverpool, Daniel Agger amedai kuwa Liverpool imekataa ofa iliyotumwa na Barcelona kwa ajili ya kumsajili mchezaji huyo. Barcelona imekuwa ikihusishwa na kutaka kusajili mabeki kadhaa wa Ligi Kuu nchini Uingereza ambapo tayari walishatoa kitita cha euro milioni 25 kwa ajili ya beki wa Chelsea David Luiz. Chelsea waliweka wazi kuwa mabingwa wa soka nchini Hispania wanapoteza muda wao na sasa wakala wa Agger aitwaye Per Steffensen naye amebainisha kuwa Liverpool tayari wamepiga chini ofa hiyo. Wakala huyo amesema mteja wake bado ana mkataba wa miaka mitatu na Liverpool hivyo ni juu ya makubaliano ya klabu hizo mbili kuhusu ada ya uhamisho.
No comments:
Post a Comment