MENEJA wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amejitetea kuhusu tuhuma za kushindwa kutumia fedha katika kipindi hiki cha usajili wa majira ya kiangazi. Mpaka sasa Arsenal imefanikiwa kumsajili Yaya Sanogo pekee huku wakishuhudia ofa zao mbili za kumsajili Luis Suarez zikikataliwa na Liverpool. Mbali na Suarez Arsenal pia imeshindwa kuwasajili baadhi ya wachezaji iliyowahitaji katika kipindi kama Luiz Gustavo aliyehamia Wolfsburg kutoka Bayern Munich na Gonzalo Higuain aliyejiunga na Napoli akitokea Real Madrid. Pamoja na hayo Wenger amesisitiza kuwa haogopi kutumia fedha kwa ajili ya usajili lakini atasajili mchezaji ambaye anadhani ataimarisha kikosi chake kwa ajili ya msimu huu. Wenger amesema tuhuma kwamba yeye anabania fedha za usajili hazina mashiko yoyote kwani hana sababu ya kufanya hivyo na kitu cha msingi ni kuhakikisha naimarisha kikosi cha ili kiweze kumaliza ukame wa miaka nane bila mataji.
No comments:
Post a Comment