Monday, September 2, 2013

ARSENAL YAMTENGEA OZIL PAUNDI MILIONI 40.

KLABU ya Arsenal imetenga kitita cha paundi milioni 40 kwa ajili ya kumsajili kiungo wa klabu ya Real Madrid, Mesut Ozil lakini wanaweza kukabiliwa na upinzani kutoka kwa Paris Saint-Germain na Manchester United katika siku hii ya mwisho ya usajili. Kiungo huyo wa kimataifa wa Ujerumani aliweka katika benchi la wachezaji wa akiba katika ushindi wa mabao 3-1 iliyopata Madrid dhidi ya Athletico Bilbao, hatua ambayo imeonyesha kutomfurahisha hivyo kudai kuondoka. Mbali na kuwekwa benchi katika mchezo huo lakini pia ujio wa Gareth Bale ambaye amevunja rekodi ya dunia katika uhamisho wake kutoka Tottenham Hotspurs nao unaonekana kumsukuma Ozil kuondoka kwa kuhofia nafasi yake katika kikosi cha Carlo Ancelotti. Arsenal tayari walianza mazungumzo Ijumaa iliyopita na wako tayari kufikia mshahara wa paundi 180,000 kwa wiki ili waweze kumsajili nyota huyo wa kiwango cha dunia na kuwapoza mashabiki wao. Hata hivyo Arsenal hawatapata kazi rahisi kwani watapambana na PSG ambao nao walionyesha nia yao ya kumtaka Ozil, lakini mchezaji huyo anataka kwenda Uingereza hivyo kuicha Arsenal na United katika kinyang’anyiro hicho.

No comments:

Post a Comment