Monday, September 2, 2013

WILLIAMS ATINGA ROBO FAINALI YA US OPEN.

MWANADADA nyota katika tenisi anayeshika namba moja katika orodha za ubora duniani kwa upande wa wanawake Serena Williams amefanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya michuano ya wazi ya Marekani kwa kumfunga Sloane Stephens. Williams ambaye ni bingwa mtetezi wa michuano hiyo alimchakaza Stephens ambaye ni Mmarekani mwenzake kwa 6-4 6-1 katika mchezo uliopigwa katika Uwanja wa Arthur Ashe jijini New York. Williams ambaye atakwaanza na Carla Suarez Navarro wa Hispania katika hatua ya robo fainali alimsifu mpinzani wake kwa kucheza vizuri hivyo kumpa wakati mgumu kwenye mechi hiyo. Kwa upande wa wanaume Novak Djokovic amefanikiwa kutinga mzunguko wan ne wa michuano hiyo kwa kumfunga Joao Sousa wa Ureno kwa 6-0 6-2 6-2. Nyota huyo kutoka Serbia ambaye ni bingwa wa michuano hiyo mwaka 2011 alimgaragaza Sousa kwa kutumia muda wa saa moja na dakika 45 na sasa atachuana na Marcel Granollers wa Hispania katika kutafuta nafasi ya kucheza robo fainali.

No comments:

Post a Comment