Thursday, September 12, 2013

BABA YAKE OZIL ATISHIA KUWAPELEKA POLISI WANAMSHUTUMU MWANAE KUPENDA KULA BATA.

BABA wa kiungo wa kimataifa wa Ujerumani, Mesut Ozil ametishia kuchukua hatua za kisheria baada ya madai ya vyombo vya habari nchini Hispania kwamba mchezaji huyo alikuwa amebanwa na mambo binafsi wakati akiwa Real Madrid. Mapema wiki hii gazeti la ABC lilimkariri rais wa Madrid, Florentino Perez akidai anaamini Ozil hakuwa mchezaji mwenye weledi kwasababu maisha yake akiwa huko yalitawaliwa na wanawake na starehe za usiku. Lakini Mustafa ambaye ndio baba yake Ozil amejibu tuhuma hizo na kudai ni za kipuuzi kwani mwanae alikuwa akijitoa wakati akiwa Madrid ndio maana alikuwa akicheza mara nyingi. Mustafa amesema wanataka kumlaumu mwanae hivi sasa kwasababu mashabiki na wachezaji wenzake wamekasirishwa na uamuzi wa klabu hiyo kumuuza. Ozil ambaye amefunga na kusaidia mabao 108 katika mechi 159 alizocheza akiwa Madrid alikamilisha umamisho wake kwenda Arsenal katika dakika za mwisho kabla ya dirisha la usajili halijafungwa wenye thamani ya euro milioni 50 na kuwashangaza wachezaji wenzake wengi.

No comments:

Post a Comment