BEKI mahiri wa klabu ya Barcelona, Gerard Pique anaamini kuwa mshambuliaji mpya wa klabu ya Real Madrid Gareth Bale anaweza kushindwa kung’ara katika miezi michache ya kwanza akiwa Santiago Bernabeu. Beki huyo wa kimataifa wa Hispania, hana shaka kwamba Bale atafanya vizuri akiwa na Madrid lakini anafikiri nyota wa zamani wa klabu ya Tottenham Hotspurs anathitaji muda ili kuzoea mazingira ya hapo na mahitaji ya klabu kubwa kama hiyo. Pigue amesema huwezi kujua jinsi gani atazoea mazingira ya vyumba vya kubadilishia nguo huku pamoja na nyota wengine wa Madrid kama Cristiano Ronaldo na Karim Benzema. Beki huyo aliendelea kutiririka kuwa mchezaji yoyote anayecheza katika klabu kubwa kama Madrid anakuwa katika msukumo mkubwa kwasababu unatakiwa kushinda kila mchezo hivyo katika mizei ya mwanzoni lazima upate tabu lakini anaamini baada ya muda atazoea. Bale anaweza kucheza mechi yake ya kwanza rasmi na Madrid Jumamosi wakati watakaposafiri kuifuata Villarreal.
No comments:
Post a Comment