Wednesday, September 11, 2013

BACH RAIS MPYA IOC.

THOMAS Bach wa Ujerumani ameteuliwa kuwa rais mpya wa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki-IOC akichukua nafasi ya Jacques Rogge wa Ufaransa. Bach, wakili mwenye umri wa miaka 59 ambaye ni bingwa wa zamani wa medali ya dhahabu katika mchezo wa fencing kwenye michuano ya olimpiki mwaka 71 amechukua nafasi ya Rogge alieongoza kamati hiyo kwa kipindi cha miaka 12. Bach ambaye anakuwa rais wa tisa katika historia ya miaka 119 toka kuanzishwa kwa IOC alikuwa mgombea anayepewa nafasi kubwa miongoni mwa wagombea sita waliokuwa wakiwania nafasi hiyo katika uchaguzi uliofanyika huko Buenos Aires, Argentina. Akihojiwa mara baada ya ushindi huo Bach aliwashukuru watu wote waliompigia kura na kudai kuwa anajua changamoto mbalimbali zitakazomkabili wakati atakapokuwa katika kiti hicho cha IOC kwa kipindi cha miaka nane ijayo.

No comments:

Post a Comment