Tuesday, September 10, 2013

BARCELONA YAINGIA MKATABA NA BENKI YA KIARABU.

KLABU ya Barcelona imekubali mkataba wa miaka mitatu na Benki ya falme za Kiarabu-UAB, ambapo mabingwa hao wa La Liga wamedai ni taasisi ya kwanza ya kibenki huko Falme za Kiarabu-UAE kudhamini klabu ya soka. Klabu hiyo haikuweka wazi makubaliano ya fedha yaliyofikiwa katika mkataba huo ambao utaishia Julai 2016 lakini imedai kuwa wateja wa UAB watakuwa wakipewa siti za upendeleo kutizama mechi za timu hiyo. Wakiwa kama wadhamni rasmi, benki hiyo inatarajiwa kutengeneza bidhaa mbalimbali zenye nembo ya Barcelona ili kukidhi matakwa ya mashabiki wengi wa klabu hiyo sehemu mbalimbali huko UAE. Barcelona imekuwa na mashabiki wengi sehemu mbalimbali duniani hususani nchi za kiarabu hivyo mkataba huo utakuwa ni fursa nzuri kwa timu hiyo kujiongezea kipato na mashabiki zaidi.

No comments:

Post a Comment