Saturday, September 14, 2013

BARCELONA INAHITAJI MABEKI - PASSARELLA.

RAIS wa klabu ya River Plate, Daniel Passarella amedai kuwa Gerardo Martino amemwambia kuwa ana nia kusajili mabeki kwa ajili ya klabu ya Barcelona katika kipindi cha usajili wa dirisha dogo Januari mwakani. Hata hivyo Passarella mwenye umri wa miaka 60 ambaye alikuwa nyota wa zamani wa Argentina, amesisitiza kuwa Martino hakumtajia amajina ya mabeki anaowahitaji katika mazungumzo yao. Nguli huyo alidai kuwa walizungumza na Martino kwa mudaa wa saa moja na kumdokeza kuwa ifikapo Desemba mwaka huu atahitaji kusajili mabeki ili aweze kuongeza nguvu katika kikosi chake. Safu ya ulinzi ya Barcelona imekuwa sio nzuri kwa kipindi kirefu lakini hivi sasa watapata ahueni baada ya nahodha wake Carles Puyol kutarajiwa kurejea mazoezi wiki ijayo.

No comments:

Post a Comment