MENEJA wa klabu ya Monaco ya Ufaransa, Claudio Ranieri amekisifu kikosi cha timu ya Paris Saint-Germain-PSG kuwa bora kuliko cha kwake lakini akatamba kuwa atafanya kila awezalo kuhakikisha wanashinda taji la Ligi Kuu ya nchi hiyo msimu huu. Monaco imepanda ligi kuu msimu huu na kufanya usajili wa nguvu kwa kuzoa wachezaji nyota kutoka sehemu mbalimbali akiwemo mshambuliaji nyota wa kimataifa wa Colombia Radamel Falcao. Hata hivyo pamoja na Monaco kukaa nyuma ya PSG kwa tofauti ya alama moja kwenye msimamo wa ligi, Ranieri hakuacha kuwasifu mabingwa hao watetezi wa ligi hiyo kwa kuwa na kikosi imara. Ranieri amesema Monaco ina kikosi kizuri lakini huwezi kufananisha na PSG kwasababu wenyewe wamekaa pamoja kwa zaidi ya miaka miwili ikilinganisha na wao ambao wamepanda msimu huu.
No comments:
Post a Comment