MSHAMBULIAJI nyota wa zamani wa kimataifa wa Italia, Alessandro Del Piero ameteuliwa kuwa nahodha mpya wa kikosi cha Sydney FC ya Australia kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu ya nchi hiyo maarufu kama A League. Nyota huyo wa zamani wa klabu ya Juventus ambaye aliweka rekodi ya usajili katika historia ya ligi ya Australia amechangia kwa kiasi kikubwa kuvutia mashabiki uwanjani pamoja na vyombo vya habari nchini humo. Kutokana na hilo Sydney imeamua kumpa unahodha katika msimu wa 2013-2014 ambao unatarajiwa kuanza kutimua vumbi Octoba akichukua nafasi ya Terry McFlynn. Del Piero ambaye pia amewahi kuwa nahodha Juventus kwa miaka 11, amesema ni heshima kubwa kwake kuwa nahodha katika moja ya klabu kubwa nchini humo na bara ya Asia. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 38 alijiunga na Sydney mwaka jana akitokea Juventus na kuvunga mabao 14 mpaka sasa.
No comments:
Post a Comment