Wednesday, September 18, 2013

KROL KUINOA TUNISIA.

SHIRIKISHO la Soka nchini Tunisia limetangaza kumpa kibarua nahodha wa zamani wa kimataifa wa Uholanzi Ruud Krol kuinoa timu ya taifa ya nchi hiyo katika mechi zake za mtoano ili kufuzu michuano ya Kombe la Dunia mwakani. Tunisia imepangwa kuchezwa na Cameroon katika mechi za mikondo miwili zitakazochezwa Octoba na Novemba wakichukua nafasi ya Cape Verde walioondolewa na Shirikisho la Soka Duniani-FIFA. Krol anachukua nafasi ya nabil Maaloul ambaye alijiuzulu baada ya Tunisia kupoteza mechi yake ya mwisho nyumbani kwa kufungwa mabao 2-0 na Cape Verde Septemba mwaka huu. Matokeo hayo yalimaanisha nchi hiyo kukosa nafasi ya kwenda hatua ya mtoano lakini walipata nafasi hiyo siku chache baadae wakati Cape Verde walipokutwa na hatia ya kumchezesha mchezaji asiyeruhusiwa na FIFA kuwapa ushindi wa mabao 3-0 uliowazesha kusonga mbele. Krol ambaye amepewa mkataba wa miezi miwili pia ataendelea kukinoa kikosi cha CS Sfaxien klabu ambayo ameiwezesha kunyakuwa ubingwa wa Ligi Kuu nchini Tunisia Mei mwaka huu.

No comments:

Post a Comment