Wednesday, September 18, 2013

MESSI HAJAOMBA NYONGEZA YA MSHAHARA - ROSELL.

RAIS wa klabu ya Barcelona, Sandro Rosell amesisitiza kuwa Lionel Messi hajaomba mkataba mpya wenye maslahi zaidi baada ya Real Madrid kumfanya Cristiano Ronaldo kuwa mchezaji anayelipwa zaidi duniani. Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ureno amesaini mkataba mpya wa miaka mitano utakaomuwezesha kukunja kitita cha euro milioni 21 kwa msimu Jumapili iliyopita na kuzusha chokochoko kuwa Messi naye atahitaji kupandishiwa mshahara ili kumfikia Ronaldo. Hata hivyo Rosell alifafanua kuwa mkataba mpya wa Ronaldo hauna athari zozote kwenye mkataba wa sasa wa Messi. Rosell amesema nyota huyo wa kimataifa wa Argentina hajazungumza lolote kuhusiana na hilo na anaonyesha kufurahia kuwepo katika klabu hiyo bora kabisa duniani.

No comments:

Post a Comment