Friday, September 13, 2013

FIFA YAITOSA DRC.

KAMATI ya nidhamu ya Shirikisho la Soka Duniani-FIFA imetupilia mbali madai yaliyotolewa na Shirikisho la Soka la Congo wakidai kuwa Niger ilichezesha mchezaji asiyeruhusiwa katika mechi ya kufuzu Kombe la Dunia baina ya timu hizo Septemba 7 jijini Niamey. Hatua hiyo ya FIFA inamaanisha kuwa Burkina Faso wanabakia kama viongozi wa kundi E hivyo kufuzu hatua ya mtoano ya michuano hiyo. Maofisa wa soka wa Congo wamedai kuwa Niger ilimtumia Mahamane Cisse ambaye uraia wake ulikuwa na matata hivyo kumfanya kukosa vigezo vya kucheza mechi hiyo. Hata hivyo FIFA walitupilia mbali madai hayo na kudai kuwa Niger hawakukiuka sheria zozote kwa kumtumia mchezaji huyo.

No comments:

Post a Comment