Friday, September 13, 2013

BRAZIL HAIPASWI KUMTEGEMEA NEYMAR PEKEE - PELE.

NGULI wa soka nchini Brazil Pele, amedai kuwa timu ya taifa ya nchi hiyo haipaswi kumtegemea mshambuliaji wake nyota Neymar moja kwa moja. Nyota huyo amekuwa mshambuliaji tegemeo kwa Brazil toka ang’are katika michuano ya Kombe la Shirikisho mapema mwaka huu huku akufunga mabao tena katika mechi mbili za kimataifa za kirafiki dhidi ya Australia na Ureno. Hata hivyo, Pele anadhani hata kama mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 ameonyesha kukomaa haipaswi kumtwisha majukumu mengi kwani inaweza kuigharimu nchi hiyo wakati watakapomkosa. Pele amesema nchi hiyo ina vipaji vingi ambavyo kocha anaweza kuvitumia bila ya kutegemea huduma ya mchezaji mmoja moja kwa moja.

No comments:

Post a Comment