SERIKALI ya Ivory Coast imetangaza kutafuta nafasi ya kuandaa michuano ya Mataifa ya Afrika mwaka 2019 au 2021. Kwa wa taarifa iliyotolewa na Shirikisho la Soka la nchi hiyo-Fecafoot, imedai kuwa serikali imewaruhusu kutuma barua ya maombi kwa Shirikisho la Soka barani Afrika-CAF. Ili kuhakikisha wanapata nafasi ya kuandaa michuano hiyo serikali ya nchi hiyo imepanga kutengeneza mazingira rafiki ikiwemo suala la kuboresha miundo mbinu yake. Mara ya mwisho Ivory Coast kupata uenyeji wa kuandaa michuano hiyo ilikuwa mwaka 1984 lakini harakati zao za kutaka kuandaa michuano ya mwaka 2006 ziligongwa mwamba kutokana na machafuko ya kisiasa yaliyokuwepo nchini humo.

No comments:
Post a Comment