Friday, September 13, 2013

QATAR WAPINGA HOJA YA KUWANYANG'ANYA HAKI ZA KUANDAA KOMBE LA DUNIA 2022.

KATIBU mkuu wa kamati ya maandalizi ya michuano ya Kombe la Dunia itakayofanyika nchini Qatar 2022 Hassan al-Thawadi amepinga hoja ya michuano hiyo kuhamishiwa katika nchi nyingine. Shirikisho la Soka Dunia-FIFA katika kikao chake kijacho wanapanga kujaribu kuhamisha michuano hiyo katika majira ya baridi ili kukwepa joto kali katika kipindi cha kiangazi nchini Qatar. Mwenyekiti wa Chama cha Soka cha Uingereza Greg Dyke amesema kuna uwezekano michuano hiyo ikahamishiwa nchi nyingine kama muda mzuri wa kucheza nchini Qatar hautakubaliwa. Lakini kauli hiyo imeonekana kupingwa vikali na Al Thawadi akisisitiza kuwa hakuna sababu ya kwanini Qatar isiandae michuano hiyo kama ilivyopangwa. Al Thawadi amesema walifanya kazi kubwa kuhakikisha wanakidhi viwango katika kutafuta nafasi hiyo na muda huohuo kuhakikisha wanatimiza ahadi walizotoa hivyo haoni sababu ya kuhamisha michuano hiyo mahali pengine.

No comments:

Post a Comment