MWENYEKITI wa Chama cha Soka cha Uingereza FA, Greg Dyke amekiri kuwa hategemei Uingereza kushinda taji la Kombe la Dunia litakalofanyika nchini Brazil mwaka ujao. Akihutubia katika mkutano jijini London, Dyke amesema kikosi cha timu ya taifa ya nchi hiyo kinapaswa kuweka malengo ya kutinga nusu fainali ya michuano ya Ulaya 2020 na kushinda Kombe la Dunia 2022. Dyke amesema kauli yake haimaanishi Uingereza haitafanya vizuri nchini Brazil lakini hadhani kama kuna mtu anafikiri watakwenda kunyakuwa kombe hilo huko mwakani kama wakifuzu. Kikosi cha Uingereza ambacho kinanolewa na Roy Hodgson kinakabiliwa na mechi mbili muhimu za kufuzu ambazo ni dhidi ya Moldova utakaochezwa kesho katika uwanja wa Wembley na mwingine dhidi ya Ukraine Jumanne ijayo huko Kiev.
No comments:
Post a Comment