MARIO Gomez amebainisha kuwa angeweza kuondoka Bayern Munich kwenda Real Madrid katika kipindi cha usajili kilichopita lakini aliamua kupiga chini ofa hiyo ili aweze kujiunga na Fiorentina ya Italia. Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani alionyesha kutokuwa katika mipango ya kocha mpya wa Bayern msimu huu na vilabu kadhaa vilionyesha nia ya kutaka kumsajili. Hata hivyo nyota huyo mwenye umri wa miaka 28 alihitaji muda mchache wa kufikiri juu ya muskabali wake wakati Fiorentina walipomfuata na kupiga chini ofa ya kwenda Madrid. Gomez amesema ni kweli Ancelotti alimfuata na kutaka kumsajili lakini baada ya kufanya mazunguzo na Fiorentina kuhusu mpango yao akajua chaguo sahihi ni kjiunga nao.
No comments:
Post a Comment