KIUNGO mahiri wa kimataifa kutoka Ghana, Kevin Prince-Boateng amesisitiza kuwa Italia sio nchi ya kibaguzi pamoja na uhamisho wake kutoka AC Milan kwenda Schalke ya Ujerumani kuhusishwa na masuala hayo. Mapema mwezi huu bwana fedha wa klabu ya AC Milan, Peter Peters alikaririwa akidai kuwa uhamisho wa kiungo huyo ulichangiwa kwa kiasi kikubwa na matukio ya kibaguzi yaliyokuwa yakimuandama mara kwa mara akiwa uwanjani. Lakini Boateng alikanusha tetesi hizo na kudai kuwa hakuondoka Milan kwa ajili ya matukio ya kibaguzi. Boateng amesema hakuondoka Italia kwa ajili ya wahuni wachache ambao wamekuwa wakiongoza vitendo vya kibaguzi na anaamini nchi hiyo sio ya kibaguzi kama watu wanavyofikiria. Mchezaji huyo amecheza Milan kwa misimu mitatu na kushinda taji moja la Serie A kabla ya kurejea nchini Ujerumani katika kipindi cha usajili wa majira ya kiangazi msimu huu.
No comments:
Post a Comment