Monday, September 30, 2013

JORDAAN RAIS MPYA SAFA.

DANNY Jordaan amechaguliwa kuwa rais mpya wa Chama cha Soka nchini Afrika Kusini-SAFA baada ya kushinda kinyang’anyiro cha uchaguzi uliohusisha wagombe wawili. Jordaan ambaye ndiye alikuwa kiongozi wa kamati ya maandalizi ya michuano ya Kombe la Dunia 2010 alipata kura 162 dhidi ya 88 za mpinzani wake katika uchaguzi huo Mandla Mazibuko. Rais aliyemaliza muda wake Kirsten Nematandani alikosa nafasi ya kushiriki uchaguzi huo baada ya mikoa wanachama 52 ya SAFA kutomchagua. Katika kipindi chake cha miaka minne, Jordaan mwenye umri wa miaka 62 anakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo masuala ya utawala, fedha na matokeo mabaya ya timu ya taifa ya nchi hiyo maarufu kama Bafana Bafana.

No comments:

Post a Comment