Thursday, September 26, 2013

JUVENTUS "YAPOZI" KUFANYA MAZUNGUZO NA PIRLO KUHUSU MKATABA MPYA.

MKURUGENZI mkuu wa klabu ya Juventus ya Italia, Giuseppe Marotta amebainisha kusimamisha mazungumzo ya kumuongeza Andrea Pirlo mpaka mapema mwakani. Kiungo huyo wa kimataifa wa Italia mkataba wake wa sasa unamalizika mwishoni mwa msimu wa 2013-2014 lakini Juventus wameonyesha kutokuwa na haraka na suala hilo. Pirlo alijiunga na Juventus kwa uhamisho huru akitokea AC Milan mwaka 2011 na ameisaidia timu hiyo kurejesha makali yake na kushinda taji la Serie A msimu uliopita huku akicheza karibu kilamechi toka kuanza kwa msimu mpya wa ligi. Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 34 hivi karibuni amesisitiza kuwa angependa kuongeza mkataba na Juventus lakini aliongeza kuwa atafanya hivyo kama akiona timu hiyo bado inamhitaji.

No comments:

Post a Comment