Thursday, September 26, 2013

QATAR YALALAMIKIWA KUWANYANYASA WAFANYAKAZI WA KIGENI.

WARATIBU wa michuano ya Kombe la Dunia 2022 nchini Qatar wamedai kushangazwa na matokeo ya uchunguzi ya jinsi wafanyakazi wa kigeni wanavyotendwa nchini humo. Kamati hiyo pia imesema serikali ya Qatar itafanyia kazi tuhuma zilizotolewa na gazeti la The Guardian kuhusiana na sakata hilo. Gazeti hilo lilidai wafanyakazi raia wa Nepal nchini Qatar wananyonywa na kunyanyaswa kwa kufanywa kama watumwa. Katika taarifa yake ofisa mkuu wa kamati hiyo ya maandalizi, Hassan Al Thawadi ameshangazwa na tuhuma hizo zilizotolewa na gazeti hilo na kudai kuwa watalifanyia uchunguzi ili kujua undani wake.

No comments:

Post a Comment