Thursday, September 26, 2013

TATIZO LA UINGEREZA SIO WAGENI NI MBINU - VIEIRA.

NGULI wa soka wa zamani wa Ufaransa, Patric Vieira amedai kuwa kushindwa kwa timu ya taifa ya Uingereza kufanya vyema katika michuano mikubwa ni suala la ufundishaji na sio wachezaji wa kigeni wanaocheza katika Ligi Kuu. Mwenyekiti wa Chama cha Soka nchini Uingereza-FA, Greg Dyke hivi karibuni alidai kuwa timu ya taifa ya nchi hiyo inahitaji wachezaji zaidi wa kiingereza ambao wanacheza mara kwa mara katika vilabu vikubwa. Lakini Vieira anapingana na kauli hiyo ya Dyke na anadhani tatizo liko ndani zaidi hapo kuliko kudai uwepo wa wachezaji wengi wa kigeni. Vieira amesema nchi hiyo inabidi kubadili mfumo wa ufundishaji ili uweze kwenda na wakati wa soka la kisasa. Nyota huyo ambaye kwasasa ni mwalimu wa kuinua vipaji katika klabu ya Manchester City amesema anadhani mchezo wa soka umebadilika kwa kiasi kikubwa hivyo hakuna jinsi inabidi na mbinu za ufundishaji pia nazo zibadilike. Uingereza haijawahi kwenda zaidi ya hatua ya robo fainali katika michuano ya Kombe la Dunia toka watinge nusu fainali mwaka 1990 na kushinda kombe hilo mara moja mwaka 1966.


No comments:

Post a Comment