Friday, September 27, 2013

BALOTELLI AOMBA RADHI.

MSHAMBULIAJI nyota wa klabu ya AC Milan, Mario Balotelli ameomba radhi kuhusiana na tukio lililopelekea kufungiwa mechi tatu kwa kuzozana na mwamuzi. Nyota huyo wa kimataifa wa Italia alifungiwa kwa kumtukana na kumtishia mwamuzi mwishoni mwa mechi ambayo Milan ilifungwa kwa mabao 2-1 dhidi ya Napoli. Balotelli alipewa kadi ya njano katika kipindi cha pili na kuongezwa kadi nyingine ambayo ilipelekea kupewa kadi nyekundu baada ya filimbi ya mwisho kupulizwa kwa kosa la kumtishia mwamuzi. Akihojiwa Balotelli aliomba radhi wachezaji wenzake na mwamuzi wa mchezo huo kwa tabia aliyoonyesha baada ya mchezo huo na kuahidi kwamba atajitahidi kudhibiti hasira zake huko mbele.

No comments:

Post a Comment