Friday, September 27, 2013

MESSI AFIKA MAHAKAMANI KUHUDHURIA KESI YAKE YA UKWEPAJI KODI.

MSHAMBULIAJI nyota wa klabu ya Barcelona, Lionel Messi na baba yake wanatarajiwa kufikishwa mahakamani nchini Hispania kujibu mashitaka ya ukwepaji kodi yanayowakabili. Nyota huyo wa kimataifa wa Argentina mwenye umri wa miaka 26 ambaye ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa dunia mara nne mfululizo na baba yake Jorge Messi wanatuhumiwa na mamlaka kwa kukwepa kodi inayokadiriwa kufikia euro milioni nne. Wote wawili wanahisiwa kutumia kampuni za nje kuuza haki za kutumia picha ya Messi kinyume cha utaratibu. Messi na baba yake walikana tuhuma tuhuma hizo ambazo zilifanyika katika kipindi cha mwaka 2007 na 2009.

No comments:

Post a Comment