Monday, September 9, 2013

KIKOSI CHA UHOLANZI BADO HAKIJAIVA KWA KOMBE LA DUNIA - CRUYFF.

NGULI wa soka wa Uholanzi, Johan Cruyff anaamini kuwa kikosi cha timu ya taifa ya nchi hiyo kinachonolewa na Louis van Gaal bado kina kazi ya kufanya kama watataka wafanikiwe katika michuano ya Kombe la Dunia mwakani. Uholanzi ilibanwa mbavu na Estonia kwa sare ya mabao 2-2 Ijumaa iliyopita baada ya kushinda mechi zake sita za kufuzu michuano hiyo na Cruyff anadhani matokeo ya wiki iliyopita yanaonyesha nchi hiyo bado haijafikia kiwango kinachotakiwa. Cruyff amesema kama nzhi hiyo ingekuwa ya kwanza barani Ulaya kufuzu bila kupoteza mchezo hilo lingeleta picha tofauti juu ya uwezo wa timu hivyo mechi dhidi ya Estonia imewashitua kuwa bado kuna kazi kubwa ya kufanya kabla ya kwenda kwenye michuano hiyo. Nguli aliendelea kudai kuwa hakuna hatari yoyote ya kushindwa kufuzu hivyo bado muda upo wa kufanyia kazi maeneo yenye mapungufu ili iweze kuwa timu imara. Uholanzi inaweza kukata tiketi kwa ajili ya Kombe la Dunia mwakani kama wakifanikiwa kuifunga Andorra baadae leo huku wakiomba Romania wanaoshika nafasi ya pili katika kundi lao wafungwe na Uturuki.

No comments:

Post a Comment