KIUNGO mahiri wa kimataifa wa Japan, Shinji Kagawa ameonyesha kuchanganyikiwa kufuatia kuenguliwa kwake katika kikosi cha Manchester United msimu huu baada ya kuifungia timu yake ya taifa katika ushindi wa mabao 3-1 waliopata dhidi ya Ghana katika mechi ya kirafiki. Kagawa ambaye mpaka sasa hajapata nafasi katika kikosi cha David Moyes msimu huu, alifunga bao maridadi la kusawazisha katika kipindi cha pili katika mechi hiyo ya kirafiki ya kimataifa. Akihojiwa mara baada ya mchezo huo, Kagawa amesema ni kitu kinachochanganya akili kukosa namba United lakini muda bado mwingi umebakia na kufunga mabao kama alivyofanya kunamfanya ajiamini zaidi. Kagawa amefunga mabao 21 katika misimu miwili aliyokuwa Borussia Dortmund lakini bado mpaka sasa hajafanikiwa kurejesha makali yake toka atue United baada ya kumaliza msimu wa kwanza akiwa amefunga mabao sita katika mechi 17 alizoanza.
No comments:
Post a Comment